Monaco wamchukua Jovetic kutoka Inter

Stevan Jovetic Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Stevan Jovetic alikaa nusu ya msimu uliopita Sevilla

Mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 Monaco wamemnunua mshambuliaji anayetoka Montenegro Stevan Jovetic kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia kwa dau la £10m.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Manchester City ametia saini mkataba wa miaka minne.

Jumatatu, picha za Jovetic, 27, akiwa amevalia jezi nambari 10 ambayo awali ilivaliwa na Kylian Mbappe zilianza kutokea mtandaoni.

Mbappe anadaiwa kukaribia kujiunga na Paris St-Germain kwa mkono.

"Nina furaha sana kuwa hapa. Kuna wachezaji wazuri sana katika timu hii. Ndio maana nikaichagua AS Monaco,2 aliambia tovuti ya Monaco.

Inaarifiwa kuwa Mbappe, 18, atajiunga na PSG kwa mkopo kabla ya dirisha la kuhama wachezaji kufungwa Alhamisi na baadaye atakamilisha uhamisho wa kudumu majira yajayo ya joto kwa euro 180m (£167m).

Mpango huo utaiwezesha kampuni hiyo ya Paris kutimiza matakwa ya sheria ya uchezaji haki kifedha baada yao kuvunja rekodi ya dunia kumnunua Neymar.

Haki miliki ya picha Saj Chowdhury

Mada zinazohusiana