Everton yakataa ombi la Chelsea kumnunua Ross Barkley

Ross Barkley
Image caption Ross Barkley

Everton wamekataa dau la £25m kutoka kwa Chelsea kumununua Ross barkley , lakini kiungo huyo wa kati wa Uingereza bado anaweza kuihama klabu hiyo kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho siku ya alhamisi.

Ombi hilo la Chelsea limedaiwa kuwa chini ya dau la £50m lililoitishwa na Everton na kwamba hakuna uwezekano wa iwapo Chelsea wataongeza dau hilo kwa kuwa mchezaji huyo amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake.

Mchezaji huyo amekataa kusaini kandarasi mpya na klabu yake ya utotoni.

Hali yake imetatizwa na jeraha baya ambalo linaweza kumweka nje kwa takriban miezi mitatu.

Chelsea wanatarajiwa kurejelea mazungumzo huku Tottenham ambao wamekuwa wakivutiwa na mchezaji huyo na wakitarajiwa kuanzisha majadiliano.

Everton pia inapima iwapo ichukue dau la chini ama impoteze mchezaji huyo bure baada ya miezi 12.

Mada zinazohusiana