Arsenal wakataa £50m za Alexis Sanchez kutoka Man City

Wenger na Sanchez
Image caption Wenger na Sanchez

Arsenal wamekataa dau ya £50m kutoka kwa wapinzani wao Ligi ya Premia Manchester City ambao wanataka kumchukua mshambuliaji nyota kutoka Chile Alexis Sanchez.

Sanchez, 28, alifungia Arsenal mabao 24 Ligi ya Premia msimu uliopita lakini mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Arsenal wamekataa majaribio yoyote ya kutaka kumchukua Sanchez kufikia sasa na wangefurahia sana iwapo Raheem Sterling atakuwa kwenye sehemu ya mkataba wake kuhamia City.

Meneja wa City Pep Guardiola inadaiwa hata hivto kwamba anataka kumnunua Sanchez, 28, moja kwa moja.

Hata hivyo, hatua ya kumnunua inaweza kutilia shaka mustakabali wa Raheem Sterling katika City.

Sterling, 22, anayechezea timu ya taifa ya England amechezea City mechi zao zote tatu za kwanza ligini msimu huu.

Lakini hatahakikishiwa nafasi ya kuanza mechi Etihad hasa baada ya kuwasili kwa Bernardo Silva kutoka Monaco.

BBC imefahamu kwamba Sterling anaweza kufurahia kwenda Arsenal na kurejea jijini London iwapo atakuwa kwenye sehemu ya mkataba wa kumchukua Sanchez.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili.

Sanchez bado hajatia saini mkataba mpya Emirates.

Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili.

Sanchez alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban £35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita.

Mapema mwezi huu meneja wa Arsenal Arsene Wenger alisema Sanchez anataheshimu uamuzi wake wa kutaka kusalia naye mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake.

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool na England Danny Murphy amesema Arsenal hawawezi kuthubutu kumwachilia.

"Wakimwacha aende watakuwa katika matatizo chungu nzima. Bado wako kwenye matatizo makubwa kwa kiasi fulani tayari.

"Alifanya kazi kwa bidii sana (mechi dhdii ya Liverpool) lakini mechi ilipoanza kuwalemea Arsenal, ungemuona alionekana kukata tamaa.

Mada zinazohusiana