Swansea wana matumaini ya kumpata Renato Sanches

Renato Sanches Haki miliki ya picha Getty Images

Swansea City wana matumaini makubwa ya kumnunua kiungo wa kati mshambuliaji wa Bayern Munich Renato Sanches kwa mkopo wa msimu mmoja.

Mreno huyo wa miaka 20 alijiunga na Bayern kutoka Benfica kwa €35m mwezi Mei mwaka 2016.

Sanches, ambaye alichezea mabingwa hao wa Ujerumani mechi 25 msimu uliopita, alikuwa pia kwenye kikosi cha Ureno kilichoshinda Euro 2016.

Mkufunzi mkuu wa Swansea Paul Clement alifanya kazi na Sanches alipokuwa meneja msaidizi Bayern.

Mkataba wowote wa uhamisho wake utahitajika kukamilishwa kabla ya dirisha la kuhama wachezaji kufungwa tarehe leo 31 Agosti.

Sanches anatazamwa kama mchezaji anayeweza kujaza nafasi ya Gylfi Sigurdsson, aliyejiunga na Everton kwa £45m tarehe 16 Agosti.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Renato Sanches alichezea timu ya taifa ya taifa ya vijaa ya Ureno mechi 40 na kuwafungia mabao manane

Mreno huyo amesalia na miaka minne katika mkataba wake Bayern.

Mada zinazohusiana