Crystal Palace wakamilisha usajili wa Mamadou Sakho kutoka Liverpool

Mamadou Sakho Haki miliki ya picha Getty Images

Crystal Palace wamekamilisha usajili wa beki wa Mamadou Sakho kutoka Liverpool kwa £26m.

Palace walifanikiwa baada ya kuwasilisha ombi lao la nne la kutaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 27.

Walikuwa wamewasilisha dau ya £25m Jumanne lakini ikakataliwa.

Liverpool awali walikuwa wamesema hawangekubali chini ya £30m kwa beki huyo wa Ufaransa, ambaye alifana sana akiwa kwa mkopo Selhurst Park msimu uliopita.

Sakho alijipata akiwa mchezaji wa ziada Anfield baada ya kutoelewana na meneja Jurgen Klopp.

Mwenyekiti wa Paris Steve Parish hatimaye alifanikiwa baada ya dau yake ya £22m na vikolezo vya £3m kukataliwa awali.

Haki miliki ya picha CPFC
Image caption Sakho kwenye video baada ya kuthibitishwa kurejea Palace alisema "mwanajeshi amerejea".

Hata baada ya kutofikisha lengo lao la £30, Liverpool bado walipata faida kutoka kwa mchezaji huyo ambaye walikuwa wamemnunua £18m kutoka Paris St-Germain Septemba2013.

Leicester City na West Bromwich Albion walikuwa pia wanamtaka lakini inaaminika mchezaji huyo alitaka kurejea London.

Palace wameanza msimu huu kwa kulazwa mechi zao zote tatu Ligi ya Premia chini ya meneja wao mpya Frank de Boer.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mamadou Sakho (kulia) amechezea timu ya taifa ya Ufaransa mechi 28

Mada zinazohusiana