Je Real Madrid itahifadhi taji lake la vilabu bingwa Ulaya?

Real Madrid wanawania ushindi wa mara ya tatu mfululizo kutaka kushinda taji la klabu bingwa Ulaya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Real Madrid wanawania ushindi wa mara ya tatu mfululizo kutaka kushinda taji la klabu bingwa Ulaya

Real Madrid wanawania ushindi wa mara ya tatu mfululizo kutaka kushinda taji la klabu bingwa Ulaya, Paris St-Germain wanavunja rekodi huku Barcelona wakionekana kudidimia.

Ukiongeza rekodi ya wagombea sita katika kikosi hicho katika msimu huu , unaotarajiwa kuanza rasmi siku ya Jumanne, unatarajiwa kuwa msimu wa kuvutia zaidi.

  • Je, Real Madrid inaweza kumiliki taji kwa mara ya tatu mfululizo?

Baada ya kuwa klabu ya kwanza kushinda kombe kwa miaka miwili mfululizo , katika ligi ya klabu bingwa ulaya, Real Madrid tayari imeweka historia.

Lakini swali ni iwapo wataweza kulitetea taji hilo kwa miaka mingi kufuatia matokeo ambayo yamekuwa wakishuhudia kutoka kwa wachezaji ambao waliwatangulia misimu mitano iliyopita na kushinda kombe la ulaya tangu kuazishwa kwa ligi hiyo mwaka 1956.

Kuna dalili nzuri za kupata ushindi.Ni mara chache ambapo timu hufuzu katika ligi ya vilabu bingwa ikiwa na kikosi kikali.

Si kwa kawaida kwamba Real katika kipindi cha pili wakati walipokuwa wakikabiliana na Juventus mwezi Juni katika fainali huko Cardiff iliwavutia wengi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu katika uwanja wa Bernabeu.

Klabu hiyo ilidhihirisha kwamba kuna mipango katika siku za mbeleni ya kuwatengemea wachezaji nyota.

Klabu hiyo imekuwa ikiwateuwa vijana wadogo wenye talanta kama Marco , Asensio, Dani Ceballos na wachezaji wengine wa klabu hiyo mbali na kocha wao Zinedine Zidane ambaye amekuwa akiwateuwa wachezaji hao kutokana na ujuzi na sio kulingana na nafasi yao katika jamii.

  • Je tunastahili kuihesabu Paris St-Germain miongoni mwa klabu zinazopendwa?

Iwapo Real Madrid wamerudi nyuma kwa kuwasajili wachezaji wakati wa uhamisho , hapo basi PSG wamejinyakulia nafasi kwa namna nyengine.

Usajili wa Neymar uliwashangaza wengi katika ulimwengu wa soka, na ilionekana kama mwanzo mpya kwa Wafaransa hao.

Kufuatia matokeo ya klabu hiyo tangu uwekezaji wa kutoka Qatar (QSI) mwaka 2011, klabu hiyo ilikuwa haijawahi kuwa na uwezo wa kufanya usajili wowote kwa wachezaji wa hali ya juu hadi hivi sasa.

Huku akishirikiana na kinda wa Ufaransa Kylian Mbappe aliyeiaga Monaco na kuelekea Parc des Princes, Neymar bado ataendelea kuwa miongoni mwa wachezaji watatu wa Ulaya lakini kwa hivi sasa mambo yatakuwa na uso mpya.Timu hiyo sasa inawashambuliaji nyota watatu Neymar, Mbappe na Edinson Cavani.

  • Je, Barcelona ni wapizani halisi?

Bidii ya Barcelona kuishinda PSG walipokuwa wakikabiliana dhidi ya PSG waliotoka sare katika hatua ya timu kumi na sita bora ilisababishwa na bidii na jitihada za Neymar.

Bado klabu hiyo imeachwa mdomo wazi baada ya raia huyo wa Brazil kuhamia Ufaransa huku shida ambazo mabingwa hao wamekuwa wakikumbana nazo uwanjani na katika vyumba vya mikutano sasa zimewekwa hadharini.

Neymar angekatazwa kuihama klabu hiyo lakini haikuwezekana kwani alikuwa amekosa matumaini na usimamizi wa Barcelona.

Lionel Messi bado hajasaini muda zaidi wa mkataba wake ambao utakamilika msimu huu, baada ya rais ambaye anakumbana na changamoto , Joseph Bartomeu kudai kwamba kiungo wa kati Andres Iniesta alitarajiwa kutia saini mkataba mpya mbele ya umma na akakataa.

  • Ni timu gani ya Uingereza itafika kileleni?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manchester United waliposhinda kombe la vilabu bingwa Ulaya

Ni msimu wa historia kwa timu za Uingereza , zikiwemo timu tano katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza , Manchester United walifuzu kupitia ligi ya Uropa na wataungana na mabingwa wa Scotland Celtic baada ya kuonyesha matamanio yao ya kujiunga na michuano hiyo.

Kikosi cha Jose Mourihno kimeonekana kurudi katika michuano hiyo na kuwa kileleni katika kundi lao, licha ya kwamba Benfica ni wapizani ambao hawastahili kudharauliwa.

Chelsea wanakumbana na Atletico Madrid huku Manchester City wakistahili kuwa macho kwa mashambulizi ya Napoli na timu ya Ukraine ya Shakhtar Donetsk, ambayo imevunja rekodi chini ya meneja Paulo Fonseca msimu uliopita.

  • Je, nani atawashangaza wengi kwa kipato chake mwaka huu?

RB Leipzig inatarajia ushindani mkali , wamewekwa katika kundi lililoko katika kiwango sawa pamoja na mabingwa wa Ufaransa Monaco, Besiktas na Porto.

Hata upande wa Ralph Hasenhuttl wamefanya kazi ngumu zaidi kwa kumtumia Naby Keita na Emil Forsberg katika safu yake ya kati.

Timo Werner atafunga mabao na winga aliyesainiwa upya Bruma ni kiungo machachari. Leipzip kwa hivi sasa wanafahamu jinsi ya kujiimarisha.

Napoli ni farasi mweusi katika hatua za hapo mbeleni.

Katika timu za ligi ya Serie A, AC Milan imeonyesha mabadiliko katika kipindi cha dirisha la uhamisho , upande wa Maurizio Sarri wameamua kuwa dhabiti na wameamua kuwatumia Dries Mertens, Jose Callejon na Lorenzo Insigne.

Huku katika kiungo cha kati wakiwa na matarajio ya kumtumia Marek Hamsik ambaye yuko karibu kufikia rekodi ya ufungaji magoli ya Diego Maradona ambayo wanajaribu kuipiku.