Kenya na Tanzania zashuka orodha ya Fifa

Tanzania
Maelezo ya picha,

Taifa Stars ya Tanzania wakipiga jaramba

Timu za soka za mataifa ya Kenya na Tanzania zimeshuka kwenye orodha ya kila mwezi ya viwango vya soka duniani inayotolewa na Fifa.

Harambee Stars imeshuka nafasi sita hadi nambari 88 duniani, Taifa Stars nao wakashuka nafasi tano hadi nambari 125.

Rwanda wamepanda nafasi moja hadi nambari 118, lakini DR Congo wameshuka nafasi 14 hadi nambari 42.

Uganda wamepanda nafasi mbili na wanashikilia nafasi ya 71.

Burundi wamepanda nafasi tatu hadi nambari 129.

Misri wanaongoza Afrika wakiwa katika nafasi ya 30 baada ya kushuka nafasi 5.

Somalia na Eritrea wanashika mkia wakiwa nafasi ya 206 kwa pamoja, wakiwa hawana alama zozote.

Ushelisheli wanawafuata kutoka nyuma wakiwa nafasi ya 190 baada ya kupanda nafasi 4.

Ujerumani sasa ndio taifa bora zaidi kwa soka duniani baada ya kuwapita Brazil ambao sasa wanashikilia nafasi ya pili.