Morocco na Kenya zawika voliboli ya walemavu Rwanda

Morocco wameilaza Afrika Kusini seti 3-0
Mashindano ya voliboli ya walemavu kuwania ubingwa wa Afrika yaliingia katika siku yake ya pili Alhamisi mjini Kigali timu ya Morocco ikiwa ya kwanza kujihakikishia tiketi ya robo fainali.Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema timu ya Morocco imeendelea kuonyesha umahiri katika mashindano hayo.
Mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita Morocco imeilima Afrika Kusini seti 3-0.Ushindi huu unafuatia ushindi mwingine wa jana Morocco ilipoizaba Kenya seti 3-0 za 25-21,25-19 na 25-18.
Mchezaji wa Kenya James Mang'erere akakiri kuzidiwa maarifa.Jana usiku pia Rwanda ilikandika Afrika kusini seti 3-0 25-10,25-16 na 25-17.Upande wa wanawake Misri ilichapwa na Kenya seti 3-2 huku Rwanda ikiichalaza DRC seti 3-0.
Rwanda waliishinda Kenya seti 3-0 baadaye jioni.
Kwa ushindi huo Rwanda imejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza nusu fainali.
Mechi nyingine ya wanaume ilishuhudia ushindi wa Misri seti 3-0.Upande wa wanawake pia Rwanda imeilima Misri seti 3-0 Kenya ikaichapa DRC seti 3-0.
Rwanda awali walicheza dhidi ya DR Congo