Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 15.09.2017

Kipa wa Manchester United David De Gea
Maelezo ya picha,

Kipa wa Manchester United David De Gea

Real Madrid inajiandaa kuimarisha hamu yao ya kutaka kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea ,26, pamoja na kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard , 26, msimu ujao. (Don Balon, via Goal)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, atakataa uhamisho wa kujiunga na Real Madrid ili kujiunga na wapinzani wa Arsenal Manchester City. (Daily Mirror)

Sanchez ni miongoni mwa washambuliaji waliorodheshwa na Real Madrid akiwemo mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski ,29, mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, 28, mbali na mshambuliaji wa Torino Andrea Balotti ,23, (Don Balon, via Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alexis Sanchez

Liverpool itajaribu kumsajili beki wa Lazio Stefan de Vrij ,25, mnamo mwezi Januari (Calicomercato, via Talksport)

Mkufunzi wa klabu ya Leicester City, Craig Shakespeare anatumai kupokea habari za hatma ya kiungo wa kati Adrien Silva ,28, ambaye usajili wake kutoka Sporting Lisbon umekataliwa na Fifa. (Daily Mail)

Mchezaji anayelengwa na Liverpool Timo Werner, 21, ameiambia klabu ya RB Leipzig kwamba anataka kuchezea klabu kubwa msimu ujao .Mshambuliaji huo anasakwa na klabu ya Real Madrid. (Bild, via Yahoo)

Maelezo ya picha,

Neymar Jr

Kitita cha uhamisho wa Neymar cha £200m kilichovunja rekodi ya dunia kutoka Barcelona hadi PSG kina thamani ya £8m ya klabu ya zamani ya mchezaji huyo Santos kulingana na rais wa klabu hiyo.(Esporte, via ESPN)

Mshambuliaji wa Tottenham Vincent Janssen ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce hakukataa uhamisho wa West Brom kwa kuwa timu hiyo haikuwasilisha ombi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa 23 (Birmingham Mail)

Maelezo ya picha,

Ricardo Rodrigues

Klabu ya Real Madrid inatarajiwa kumsajili kinda Ricardo Rodrigues ,17, kutoka klabu ya Gremio Novorizontino katika kandarasi ya miaka 6 (AS, via Daily Star)

Klabu ya Manchester United imekubali kumsajili kinda Charlie McCann kutoka klabu ya Coventry (Daily Mail)

PSG imemuongezea kandarasi kinda wa zamani wa Barcelona Kays Ruiz ,15, kwa kandarasi ya chipukizi ya hadi 2020 (ESPN)