Gennady 'GGG' Golovkin kuzipiga dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez

Gennady 'GGG' Golovkin kuzipiga dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez
Maelezo ya picha,

Gennady 'GGG' Golovkin kuzipiga dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez

Pigano la uzani wa middleweight kati ya Gennady 'GGG' Golovkin dhidi ya Saul 'Canelo' Alvarez limetajwa kuwa la aina yake ikilinganishwa na lile lililodaiwa kuwa na mbwembwe kati ya Floyd Mayweather na bingwa wa UFC Conor McGregor.

Tayari tiketi zote za pigano hilo la Jumamosi zimeuzwa kwa £18,000 kila moja huku mataji mawili ya uzani wa middleweight yakipiganiwa na kuwa mojawapo ya mapigano yaliotarajiwa na wengi mjini Las Vegas.

Maelezo ya picha,

Pigano kubwa kati ya Canelo Alvarez dhidi ya GGG wikendi

Canelo Alvarez ambaye ameshindwa mara moja pekee katika mapingano zaidi ya 50 aliyoshiriki huku GGG akiwa hajashindwa katika mapigano yake yote na ndiye anayeshikilia mataji ya IBF na IBC katika uzani huo.

Pigano hilo litafanyika siku ya Uhuru wa Mexico hivyobasi ushujaa wa Alvarez unatarajiwa kupigwa jeki siku hiyo.

Kulingana na duru za pigano hilo Alvarez amelitaja kuwa pigano 'hatari' zaidi katika historia ya mapigano aliyoshiriki.

Hii ni taarifa yenye maana kubwa kwa bondia wa umri wa miaka 27 ambaye ameipigana ndondi za kulipwa kwa takriban miaka 12 huku akipoteza pigano moja pekee kwa aliyekuwa bingwa wa zamani katika uzani huo Floyd Manny Mayweather 2013.

Hatahivyo Canelo ambalo jina lake linamaanisha 'mdalasini' kutokana na nywele zake nyekundu alikuwa akivutia wengi kwani pigano lake la Mayweather limetajwa kuwa pigano la tatu kuu lililovutia kiwango cha juu cha watazamaji katika historia ya mchezo huo.

Maelezo ya picha,

Idadi ya mapigano ya kulipwa kabla ya Alvarez kufikisha miaka 16

Hivi majuzi mapigano yaliouzwa kwa kiwango cha juu ni pamoja na lile la kati ya Andre ward na Sergey Kovalev, mbali na lile la Golovkin dhidi ya Daniel Jacobs lakini hayakuvunja rekodi .

Alvarez anatarajiwa kupokea kitita kikubwa cha fedha na anatarajiwa kupata $15m kabla ya marupurupu ya watazamaji kuongezwa.

Hayo yatakuwa mapato makubwa katika historia yake ikilinganishwa na $60 alizolipwa wakati wa pigano lake la kwanza akiwa na umri wa miaka 15 nchini Mexico 2005.

Lakini Golovkin hajawahi kupigwa knockout na hajawahi kupigwa.

Ameshinda kwa njia ya knockout mara 33 kati ya mapigano 37 aliyoshiriki, na hiyo ndio sababu Alvarez amelija pigano hilo kuwa hatari zaidi.

Mabondia waliopigana na Golvkin kama vile Kell Brook, Martin Murray, Matt Macklin wanasema lazima ujiandae kupokea makonde mazito.

Maelezo ya picha,

Makonde ya GGG ni mazito kama vile ya bondia wa uzani wa Lightheavy

Utafiti uliofanywa na chombo cha habari cha ESPN umebaini kwamba bondia huyo wa Kazakhstan ana nguvu sana.

Mbali na hilo ni mwepesi wa kurusha makonde ikilinganishwa na mbondia wengine katika uzani wa middleweight.

Hilo linamfanya kuorodheshwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi dhidi ya wapinzani wake.

Lakini sasa akiwa na umri wa miaka 35, baadhi katika ulingo wa ndondi wanaamini mechi yake ya mwisho dhidi ya Daniel Jacobs hakuonyesha kasi yake ya mchezo huo .

Ni mara ya kwanza katika takriban miaka minane ambapo GGG alihitaji usaidizi wa majaji kuweza kushinda.

Kwa upande wake Golovkin amesema wazi kwamba ndio pigano lake lililo na changamoto kuu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Canelo Alvarez alipoteza pigano moja kwa Floyd Mayweather kati ya mapigano 51 aliyoshiriki

Alikosa sherehe ya kuzaliwa kwa mwanawe wa pili hivi majuzi kutokana na mazoezi aliyokuwa akifanya kujiandaa kwa pigano hili.

''Nataka kushinda pigano hilo kwa sababu ushindi wake utakuwa wa kihistoria, kama vile mapigano mengine zaidi, kama vile lile la Sugar Ray dhidi ya Marvin Hagler na mengine mengi wakati huo''.