Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne yakumbwa na ghasia

Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne yakumbwa na ghasia
Maelezo ya picha,

Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne yakumbwa na ghasia

Mechi ya Arsenal dhidi ya Cologne katiika kombe la Yuropa ilikumbwa na ghasia na kusababisha kucheleweshwa kwa saa moja.

Maelfu ya mashabiki wa kigeni waliwasili katika uwanja huo bila tiketi na kulikuwa na ghasia kati ya mashabiki na wapokezi wao ndani ya uwanja huo baada ya mlango kufunguliwa.

Maafisa wa polisi walisema kuwa watu watano walikamatwa kwa tuhuma kuhusika katika ghasia.

Kulikuwa hakuna ripoti zozote za ghasia wakati wa mechi hiyo ambayo Arsenal ilishinda 3-1.

Timu hiyo ya Ujerumani ilikuwa imepewa tiketi 2,900 pekee.

Maelezo ya picha,

Mashabiki wa klabu ya Cologne wakiingia katika uwanja wa Emirates

Lakini takriban mashabiki 20,000 wa timu hiyo waliingia na kusimamisha biashara mjini London nyakati za mchana Alhamisi.

Hatahivyo hivyo mechi hiyo ilianza baada ya kucheleweshwa kwa saa moja.