Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 16.09.2017

Inter Milan inatumai itafanikiwa kumsajili kiungo wa kati wa PSG Adrien Rabiot anayesakwa na Arsenal pamoja na Tottenham Hotspurs
Maelezo ya picha,

Inter Milan inatumai itafanikiwa kumsajili kiungo wa kati wa PSG Adrien Rabiot anayesakwa na Arsenal pamoja na Tottenham Hotspurs

Inter Milan inatumai itafanikiwa kumsajili kiungo wa kati wa PSG Adrien Rabiot anayesakwa na Arsenal pamoja na Tottenham Hotspurs. (Calciomercato, via Talksport)

Rais wa Barcelona Josep Bartomeu anasema kuwa Lionel Messi tayari ameanza kucheza chini ya masharti ya kandarasi yake mpya na klabu hiyo hata iwapo mchezaji huyo ,30, Hajatia saini kandarasi hiyo mpya. (8TV, via Sun)

Maelezo ya picha,

Dele Alli, 21,

Mkufunzi wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa kiungo wa kati Dele Alli, 21, anahitaji kuangalia mchezo wake wakati huu ambapo klabu sita kubwa za soka zinajaribu kutaka kumsajili. (Telegraph)

Beki wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, anasema kuwa analenga kuishindia mataji klabu yake ya Spurs huku babake mchezaji huyo wa Ubelgiji na ajenti wakiendelea na mazungumzo ya kandarasi yake. (Talksport)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner yuko tayari kujiunga na klabu ya Uingereza

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner yuko tayari kujiunga na klabu ya Uingereza , lakini Real Madrid wanaweza kuwa wapinzani wa klabu yoyote inayosaka saini ya mchezaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 21. (Don Balon, via Daily Star)

Beki wa Everton Michael Keane, 24, anasema kuwa klabu yake ya zamani Manchester United ilikuwa na hamu kubwa ya kumsajili msimu uliopita lakini akaamua kueleka Goodison Park kutoka Burnley ili kushiriki mechi nyingi kwa kuwa hakuwa akiipendelea Manchester United. (Times - subscription required)

Maelezo ya picha,

PSG Julian Draxler, 23, anataka kuelekea Barcelona baada ya kupoteza nafasi yake kwa Neymar

Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 26, anasema kuwa mchezaji mwenza wa Ubelgiji na kipa wa Chelsea Thibaut Courtois, 25, atakuwa mchezaji mzuri wa zaida iwapo atajiunga na klabu hiyo ya Ufaransa (La Parisien, in French)

Wakati huohuo mshambuliaji wa PSG Julian Draxler, 23, anataka kuelekea Barcelona baada ya kupoteza nafasi yake kwa Neymar lakini ni vigumu kwa yeye kuhamia katika klabu hiyo mwezi Januari kwa sababu tayari amewahi kuichezea PSG katika kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Celtic msimu huu. (Don Balon, via Daily Express)

Manchester United inafaa kumsajili beki wa Real Madrid Varane, 24, mshambuliaji wa Borussia Dortmund's na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, kulingana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Louis Saha. (Daily Mirror)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 24, anasema kuwa Manchester United walikuwa wakimhitaji msimu uliopita lakini alipendelea kuondoka Real Madrid kuelekea Chelsea

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata, 24, anasema kuwa Manchester United walikuwa wakimhitaji msimu uliopita lakini alipendelea kuondoka Real Madrid kuelekea Chelsea (Daily Mail)

Kipa wa Stoke Jack Butland anaamini anaweza kuwa kipa wa kwanza Uingereza akiendelea kuichezea timu hiyo, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24-year- pia angependelea kushiriki katika soka ya vilabu bingwa (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Ujerumani Thomas Muller, 28, amekiri kwamba alitaka kuondoka katika klabu hiyo ya Bundelsiga na kujiunga na Manchester United 2015. (Kicker, via Independent)

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho wa Manchester United

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ametuma maajenti kumchunguza mchezaji wa Benfica na winga wa Serbia Andrija Zivkovic, 21. (O Jogo, in Portuguese)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anaamini kwamba beki na nahodha Jamaal Lascelles, 23, atatia saini ya kuongeza muda wake katika klabu hiyo hivi karibuni (Newcastle Chronicle)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anahofia kiungo wa kati Brahim Diaz, 18, anaweza kuvutiwa na Real Madrid. (Daily Express)

Maelezo ya picha,

Benjamin Mendy, 23

Mchezaji wa Manchester City na beki wa kushoto wa Ufaransa Benjamin Mendy, 23, hangetoka Monaco iwapo Chelsea ndio ingekuwa chaguo lake la pekee kulingana na rais wa Monaco Vadim Vasilyev. (L'Equipe, via Independent)

Wamiliki wa Kichina wa klabu ya West Brom's wamekataa ombi la wawekezaji wa Marekani kuinunua klabu hiyo.(Bloomberg)

Everton watalazimika kusajili mshambuliaji katika dirisha la uhamisho mwezi Januari ili kuwa na nafasi nzuri ya kufuzu katika kombe la Yuropa kulingana na kiungo wa kati wa zamani nchini Uingereza Owen Hargreaves. (BBC Radio 5 live In Short)