Hamilton ashinda michuano ya Singapore Grand Prix

Hamilton anasema sio jambo rahisi kushinda mbele ya madereva mahiri kama Vettel
Maelezo ya picha,

Hamilton anasema sio jambo rahisi kushinda mbele ya madereva mahiri kama Vettel

Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda michuano ya Singapore Grand Prix mbele ya mpinzani wake mkubwa Sebastian Vettel.

Licha ya kushinda,Hamilton anataja michuano ya mwaka huu kuwa na upinzani mkali.

Hamilton, ambaye alianza mzunguko wa tano kwa kusuasua aliongoza baada ya Vettel kugongana na dereva mwenzake wa Ferrari Kimi Raikkonen.

Maelezo ya picha,

Ni mara ya kwanza kwa magari ya Ferrari kugongana katika mbio moja

Zilikuwa ni mbio za aina yake, alisema Hamilton .

''Vettel alitarajiwa kushinda lakini kwa kutereza kwake basi nikawa mshindi''

Hamilton ameshinda kwa alama 28.