Tetesi za soka Ulaya Jumanne 19.09.2017

Kocha wa Chelsea Antonio Conte na mshambuliaji wa klabu hiyo Diego Costa
Maelezo ya picha,

Kocha wa Chelsea Antonio Conte na mshambuliaji wa klabu hiyo Diego Costa

Atletico Madrid wameipatia Chelsea kitita cha £57m kumsajili mshambuliaji Diego Costa (Marca via Talksport)

Kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 21, hafanyi mazungumzo yoyote na klabu hiyo kuhusu kandarasi mpya kulingana na meneja Mauricio Pochettino. (Daily Express)

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini, 29, bado hajaamua kuandikisha kandarasi mpya kwa kuwa ajenti wake anataka makubaliano mapya yalioimarika. (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini, 29, bado hajaamua kuandikisha kandarasi mpya kwa kuwa ajenti wake anataka makubaliano mapya yalioimarika. (Daily Mail)

Sunderland imesema kuwa uuzaji wa £30m wa Jordan Pickford, 23, hadi Everton msimu wa joto ulihitajika kuimarisha operesheni za klabu hiyo. (Daily Mirror)

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka West Ham kuwasilisha ombi jipya baada ya kushindwa kuanzishwa katika kikosi ha kwanza cha Arsenal (Daily Star)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka West Ham kuwasilisha ombi jipya baada ya kushindwa kuanzishwa katika kikosi ha kwanza cha Arsenal (Daily Star)

Manchester City wanajaribu kumsajili kiper Berke Ozer kutoka klabu ya Uturuki ya Altinordu. (Turkish-Football.com)

Maelezo ya picha,

Gabriel Jesus wa Manchester City

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus 20 , ambaye analipwa £70,000 kwa wiki anatarajiwa kuongezewa mshahara kutokana na mchezo wake mzuri katika kipindi cha miezi tisa aliyoichezea klabu hiyo.(Daily Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, ameipatia pigo Paris St-Germain akisema kuwa atarudi nchini Ufaransa kuichezea klabu yake ya zamani Lille. (SFR Sport, via Metro)

Klabu za ligi ya Premia zinatumai kutumia fursa ya kufungwa kwa shule ya soka ya klabu ya Huddersfield ili kuwasajili baadhi ya kinda wake bure.(Daily Mail)

Maelezo ya picha,

Eden Hazard wa Chelsea

Derby County inaweza kumsajili kiungo wa kati Joe Ledley, 30, ambaye ni ajenti huru baada ya kuondoka Crystal Palace katika msimu wa joto. (Derby Telegraph)

Beki Rolf Feltscher, 26, ameondoka klabu ya Birmingham City ambapo amekuwa akifanya mazoezi kwa lengo la kutaka kupata kandarasi. Kuondoka kwake kunafuatia kufutwa kazi kwa meneja Harry Kidnapp (Birmingham Mail)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Steve Cotterill yuko tayari kurudi klabu ya Birmingham kama meneja, licha ya kutengwa wakati Redknapp alipochukua kazi hiyo mbele yake msimu uliopita. (Daily Mirror)

Port Vale inataka kumsajili mkufunzi wake wa zamani Micky Adams kama mkurugenzi wa soka (sentinel)

Maelezo ya picha,

Wachezaji Sanchez na Ozil wa Arsenal

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal walifurahia kutoshirikishwa kwa wachezaji Alexis Sanchez na Messut Ozil katika timu hiyo wakati wa sare ya bila kwa bila dhidi ya Chelsea kulingana na Rory Smith wa gazeti la The New York Times newspaper. (BBC Radio 5 live)

Manchester City itaanzisha mazungumnzo na Kevin de Bruyne, 26, kuhusu kandarasi mpya na kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji anaweza kuongeza mshahara wake wa £6m maradufu (Daily Telegraph)

Maelezo ya picha,

Robert Lewandowsky

Manchester City wanataka kumsajili mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowsky,29, huku meneja Pep Guradiola akisubiri kuunganishwa na mchezaji huyo mnamo ,mwezi Januari. (Sun)

Real Madrid wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, kuhusu uhamisho mnamo mwezi Januari, lakini wachezaji waandamizi katika klabu hiyo wanasema kuwa hawamtaki mchezaji huyo.(Don Balon - in Spanish)

Mshambulaiji wa Tottenham Fernando Llorente, 32, anasema kuwa alipewa kandarasi mpya katika klabu ya Swansea lakini hakuweza kukataa uhamisho wa kujiunga na Spurs. (Wales Online)