Panama yatangaza siku kuu baada ya kufuzu kwa Kombe la Dunia

Panama's coach Dario Gomez celebrates with Roman Torres after Panama qualifies to the World Cup for the first time Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha wa Panama Dario Gomez (samawati) akisherehekea na Roman Torres baada ya kuwashinda Costa Rica t

Rais wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku kuu baada ya nchi hiyo kufuzu kwa mechi za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanaa kabisa.

Juan Carlos Varelaā€¸ aliandika katika Twitter, "Sauti za watu zimesikika...Kesho ni siku ya kitaifa."

Panama ilishinda Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City siku ya Jumanne.

Rais alisema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa.

Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo.

Haki miliki ya picha AFP/ Getty Images
Image caption Kulikuwa na shangwe katika mji wa Panama City

Hata hivyo kumekuwa na utata ikiwa goli la kwanza la Panama lilivuka mstari wa goli.

Panama imejaribu kufuzu kwa kila kombe la dunia tangu mwaka 1978 lakini haijafanikiwa hadi sasa.

Nchi hiyo itashiriki katika mechi za mwaka 2018 ambazo zinaanza Urusi mwezi Juni mwaka ujao.

Marekani ilikuwa katika kundi moja la kufuzu kwa nchi za kaskazini na kati mwa Marekani, lakini ikashindwa baada ya kupoteza kwa Trinidad and Tobago.

Mexico na Costa Rica na walifuzu.

Mada zinazohusiana