Mtangazaji wa mpira akasirika na kuondoka mechi ikiendelea

Mtangazaji wa mpira akasirika na kuondoka mechi ikiendelea na kuwawacha watazamaji vinywa wazi Haki miliki ya picha TOMIX-V
Image caption Mtangazaji wa mpira akasirika na kuondoka mechi ikiendelea na kuwawacha watazamaji vinywa wazi

Mtangazaji mmoja wa mpira nchini Urusi alikasirishwa na refa aliyekuwa akisimamia mechi moja na kuondoka katikati ya mechi hiyo na hivyobasi akawaacha watazamaji kuangalia mchezo huo bila maelezo.

Wakati wa mechi hiyo kati ya klabu ya Urusi ya Torpedo Vladmir dhidi ya Tekstilshchik Ivanovo kipa wa Ivanovo alimuangusha mshambuliaji wa upinzani kulingana na kanda za video.

Wakati huo timu hizo mbili zilikuwa 1-1.

Na badala ya kutoa mkwaju wa penalti refa alitoa mkwaju wa adhabu nje ya eneo hatari na kusababisha malalamishi kutoka kwa mashabiki na watazamaji .

Hatua hiyo ilimkasirisha mtangazaji huyo na kuamua kusitisha matangazo aliyokuwa akitoa kulingana na ripoti za Pravda.

Na wakati mkwaju huo wa adhabu ulipopigwa mmoja ya walinzi waliunawa mpira na kuzua madai ya mkwaju mwengine wa penalti lakini refa aliwaambia wachezaji kuendelea na mchezo hatua ilimlazimu mtangazaji huyo kumshutumu vikali refa huyo.

Haki miliki ya picha TOMIX TV
Image caption Kanda ya video ilionyesha kipa akimwangusha mshambuliaji

Na baada ya shutuma hizo ambapo mtangazaji huyo alimtaja bwana Nikolsky kuwa ''aibu kubwa kwa soka ya Urusi '', aliinuka na kuondoka huku akisema tazameni mechi bila mtangazaji leo .

Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1-1.