Tottenham: Guardiola 'ametukosea heshima'- Pochettino

Mauricio Pochettino na Harry Kane Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Kane amefunga 'hat trick' mara sita mwaka 2017

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema tamko la Pep Guardiola kuhusu hatua ya klabu hiyo kumtegemea sana Harry Kane ni ya "kuwakosea heshima" na ya "kusiktiisha".

Meneja huyo wa Manchester City alieleza Spurs kama "timu ya Harry Kane" alipokuwa akiwazungumzia wapinzani hao wao ligini.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 11 katika mechi saba alizochezea Spurs msimu huu.

"[Guardiola] alikuwa sehemu kubwa ya ufanisi mkubwa Barcelona na sikuwahi kusema kwamba ilikuwa 'timu ya Lionnel Messi," alisema Pochettino Ijumaa.

Guardiola aliwataja Chelsea na Manchester United kama wapinzani wakuu katika kinyang'anyiro cha kushinda Ligi ya Premia msimu huu mapema mwezi huu, kisha akaongeza: "Tuliona tena ile timu ya Harry Kane hufunga kila siku magoli mawili au matatu."

Pochettino alisema Guardiola alikuwa amefurahia zaidi baada ya ushindi wao dhidi ya Chelsea na akatania kwamba alitatizika "kudumisha sifa zake kwama mwanamume mstaarabu".

"Hainidhuru kwa vyovyote lakini kwa kweli ilikuwa ni kuwakosea heshima watu wengi," meneja huyo kutoka Argentina alisema.

"Kila mtu anahitaji kutambuliwa."

Tottenham watakutana na Bournemouth uwanjani Wembley Jumamosi.

Mada zinazohusiana