Tetesi za soka Ulaya Jumanne 17.10.2017

Real Madrid ina panga kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane kwa kitita Cha £150m (Daily Mirror).
Image caption Real Madrid ina panga kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane kwa kitita Cha £150m (Daily Mirror).

Real Madrid inapanga kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane kwa kitita Cha £150m (Daily Mirror).

Hatahivyo Tottenham itahitaji kulipwa £200m kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza.

Real Madrid itamuhitaji mshambulaiji wa Manchester United Marcus Rashford , 19, iwapo hawatamsajili Kane.(Don Balon - in Spanish)

Image caption Marcus Rashford

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atashindana na klabu yake ya zamani Barcelona kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Julian Weigl. (AS - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, anakaribia kuondoka Arsenal wakati dirisha la uhamisho la mwezi Januari litakapofunguka huku The Gunners wakitafuta mnunuzi mzuri. (Daily Mirror)

Image caption Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anapanga kumuuza Michy Batshuayi, 24,

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anapanga kumuuza Michy Batshuayi, 24, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku akimsaka mchezaji wa ziada wa mshshambuliaji Alvaro Morata, 24. (Daily Telegraph)

Beki wa kati wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, anasema kuwa hakujakuwa na maendeleo yoyote kuhusu kandarasi mpya na klabu hiyo. (Sun)

Newcastle inataka kumsajili mshambuliaji wa Besikitas Cenk Tosun mnamo mwezi Januari kwa dau la £15m.

Image caption Mchezaji wa Besikitas Cenk Tosun

Mchezaji huyo wa Uturuki , 26, pia amevutia vilabu vya Tottenham na Crystal Palace. (Daily Star)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kuongezwa donge nono la mshahara ili kuweza kutia saini kandarasi mpya.(Guardian)

Meneja wa klabu ya Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca anasema kuwa anataka kufanya kazi katika ligi ya Uingereza hatua ambayo inaweza kuishinikiza klabu ya Everton kumsaka(Daily Telegraph)

Image caption Mkufunzi wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino atataka kutia saini kandarasi ya miaka 15 na klabu hiyo ya London kaskazini (London Evening Standard)

Mkufunzi wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino atataka kutia saini kandarasi ya miaka 15 na klabu hiyo ya London kaskazini (London Evening Standard)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani, 30, anataka kuelekea Manchester City baada ya mgogoro na mshambuliaji mwenza Neymar kuzua switofahamu kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa Uruguay (Don Balon, via Manchester Evening News)

Beki wa kushoto wa Chelsea Marcos Alonso, 26, anasakwa na Barcelona .

Image caption Jordi Alba

Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid anatarajiwa kuchukua mahala pake Jordi Alba, 28 (Daily Mail)

Kipa wa Juventus Wojciech Szczesny, ambaye alikuwa akiichezea Arsenal anasema kuwa anataka kuwa mwanamitindo wa urembo wa nyumbani wakati atakapostaafu katika soka.(Independent)

Winga wa Chelsea Victor Moses anatarajiwa kuwa nje kwa takriban wiki nne akiuguza jeraha la nyuma ya goti. (Daily Telegraph)

Image caption Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Louis van Gaal anasema kuwa mrithi wake ni mtu mwenye huruma lakini alishangazwa vile alivyowachishwa kazi ESPN, via Ziggo Sport)

Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United Louis van Gaal anasema kuwa mrithi wake ni mtu mwenye huruma lakini alishangazwa vile alivyowachishwa kazi ESPN, via Ziggo Sport)

Paris St-Germain itamlipa mshambuliaji wa Brazil Neymar £2.67m) iwapo atashinda taji la mchezaji bora duniani Ballon d'Or. (Le Parisien - in French)

Image caption Marc Overmars

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, winga Marc Overmars, ambaye ni mkurugenzi wa soka katika klabu ya Ajax ,anatarajiwa kurudi katika klabu ya Gunners na kuchukua wadhfa huohuo.(Daily Star)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amefeli kuidhinisha madai ya mshambuliaji Cristiano Ronaldo, 32, ya kumshinda Messi katika kushinda taji la mchezaji bora Ulaya (Daily Express)

Mada zinazohusiana