Mourinho akana kutaka kuhamia PSG licha ya kuisifu klabu hiyo

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amekana uvumi unaoenea kwamba huenda akahamia PSG. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amekana uvumi unaoenea kwamba huenda akahamia PSG.

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amekana uvumi unaoenea kwamba huenda akahamia PSG.

Raia huyo wa Ureno aliambia chombo cha habari siku ya Jumapili kwamba hatomaliza kazi yake ya ukufunzi katika uwanja wa Old Trafford na kwamba ni kocha mwenye maono na kwamba anapendelea kufanya mambo mapya.

Alipoulizwa kuhusu matamshi yake siku ya Jumanne alisema kwamba haondoki.

''Sitatia saini kandarasi ya miaka mitano na kwamba sitohamia PSG'', alisema Mourinho mwenye umri wa miaka 54.

Katika mahojiano ya Jumapili, Mourinho ambaye aliisifu klabu hiyo ya Ufaransa na kwamba mwanawe alipendelea kwenda kutazama mechi ya klabu hiyo badala ya ile ya Manchester United.

Kwa nini Paris? Kwa kuwa kuna kitu maalum. Mchezo mzuri, ubora, ujana ni vitu vya ajabu , alisema.

Akizungumza kabla ya mechi ya vilabu bingwa ugenini Benfica, Mourinho alijibu kwamba vyombo vya habari vya Uingereza vina jibu.

''Kwa sababu kwa siku moja ninaambiwa kwamba nitatia saini kandarasi ya miaka mitano ilio na thamani ya £1bn na siku nyengine munasema kuwa ninaondoka na kuelekea PSG''.

Nadhani hilo ndio jibu, jibu ni kwamba hakuna kinachofanyika. Mourinho ambaye yuko katika msimu wake wa pili na Red Devils hajawahi kufanya kazi kwa zaidi ya miaka minne katika klabu moja.

Mada zinazohusiana