Real Madrid yazuiwa na Tottenham Bernabeu

Tottenham ilifunga bao lake la kwanza dhidi ya Real Madrid baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi nne Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tottenham ilifunga bao lake la kwanza dhidi ya Real Madrid baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi nne

Tottenham Hotspur ilionyesha kwamba inaweza kucheza katika kiwango cha juu , alisema mshambuliaji Harry Kane baada ya timu yake kupiga hatua kubwa katika kombe la vilabu bingwa kwa kujipatia alama moja ugenini Real madrid.

Spurs iliwalazimu mabingwa hao mara 12 wa Ulaya kupigania sare ya 1-1 katika uwanja wa Bernabeu siku ya Jumanne.

Timu hiyo ya ligi ya Uingereza iliongoza pale Beki wa Madrid Raphael Varane alipolazimika kujifunga kufuatia krosi ya Serge Aurier.

Mabingwa hao wa Uhispania hatahivyo walisawazisha kabla ya kipindi cha kwanza wakati Aurier alipomchezea visivyo Toni Kroos katika eneo hatari na kusababisha penalti iliofungwa na Cristiano Ronaldo.

''Alama moja katika uwanja wa Bernabeu, inaonyesha hatua tulizopiga kama timu'' , alisema Kane mwenye umri wa miaka 24.

''Tunafurahi. Ukweli wni kwamba ijapukuwa walikuwa na fursa tulicheza vizuri na kuwazuia''.

Mada zinazohusiana