Ellington: Bado napata maumivu makali miezi 10 baada ya ajali

Ellington anasema ajali hiyo nusura ichukue uhai wake
Image caption Ellington anasema ajali hiyo nusura ichukue uhai wake

Mruka viunzi wa Uingereza James Ellington amesema bado anapata maumivu makali miezi 10 baada ya ajali ya pikipiki ambayo karibia ingemuua.

Ellington alivujika mguu, pamoja na kupata jeraha kubwa kichwani wakati pikipiki yake ilipogongwa na gari mjini Tenerife mwezi januari.

Image caption Madaktari wanasema maumivu yake yataanza kupungua baada ya mwezi mmoja kutokea sasa

Mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara tatu na muda wote huo amekuwa akitembea kwa kutumia kiti cha magurudumu.

Mpaka sasa Ellington hawezi kutembea kwa kutegemea mguu wake kutokana na kutokuwa bado katika hali nzuri.

Image caption Ellington akionyesha sehemu ya kichwa aliyopata jeraha na baadaye kushonwa

Madaktari wanaomuhudumia wanasema maumivu yake yataanza kupungua mwezi ujao.

Majeraha hayo yalimfanya ashindwe kushiriki michuano ya dunia yaliyofanyika mjini London mwezi Agosti.