Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 19.10.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24, na kiungo wa kati Christian Eriksen, 25, walikuwa wakitazamwa na Barcelona wakati wa mechi na Real Madrid. (Mundo Deportivo via TalkSport)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho, amefanya mazungumzo ya mkataba mpya lakini hana mbio za kuusaini mkataba huo. (ESPN)

Leicester City hawana mbio ya kumuajiri Meneja mpya wakati wakitafuta jina kubwa kuchukua mahala pa Craig Shakespeare ambaye alifutwa siku ya Jumanne. (Daily Mirror)

Sam Allardyce amesema hana nia ya kuchukua nafasi iliyoachwa huko Leicester lakini angependa kuongoza timu ya Marekani. (TalkSport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sam Allardyce

Southampton ndiyo klabu ya kwanza kutuma ombi la kumnunua mlinzi wa Naples Kalidou Koulibaly,26, msimu huu licha ya vilabu vingine kummezea mate (Calcio Mercato - Italian)

Juventus wamejiunga na Barcelona na Manchester City kumwinda mchezasafu ya kati wa Borussia Dortmund Julian Weigl, 22.(CalcioNews24 via TalkSport)

Meneja wa Reading Jaap Stam, amethibitisha kuwa klabu hiyo ina mopango ya kumsaini mshambuliaji wa Manchestet United James Wilson, 21 msimu unaokuja. (Reading Chronicle)

Inter milan wanamfuatilia mchezaji wa Manchester City Brahim Diaz, 18. (Tuttosport via TalkSport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thomas Lemar

Arsenal na Liverpool wamebaki na nafasi nzuri ya kumwinda mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 21, baada ya Buyern Munich kujiondoa (football.london via Kicker)

NewCastle na Stoke wanewatuma maajenti kumtazama mashambuliaji wa miaka 19 Nordine Ibouroi, ambaye anachezea klabu isiyo katika ligi ya Ufarasa ya FC Martigues. (The Sun)

Mchezaji wa safu ya kati Rafinha, 24, ambaye anawindwa na Arsenal na pia Chelsea hana mipango ya kuihama Barcelona. (TalkSport)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Thomas Meunier

Aston Villa waliamua kumlipa mlizni wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 26, pesa zaidi kuliko za klabu hiyo ya Ufaransa wakati alihama mwaka 2016 (Birmingham Mail via SportFoot)

Kipa wa West Ham Adrian San Miguel, 30, ana nia ya kuondoka kutoka klabu hiyo mwezi Januari, baada ya kupoteza nafasi hiyo kwa Joe Hart. (Marca - English)

Manchester United wameanzisha mazungumzo ya mkataba na mlinzi Phil Jones, 25. (ESPN)