Wakuu wa zamani wa riadha wakamatwa kwa rushwa

Papa Massata amesema tuhuma hizo ni sawa na fitina
Image caption Papa Massata amesema tuhuma hizo ni sawa na fitina

Mkuu wa zamani wa wa shirikisho la riadha ulimwenguni Lamine Diack na mwanae Papa Massata wamekamatwa nchini Brazil kwa tuhuma za rushwa.

Tiyari wanashutumiwa kwa tuhuma kama hizo nchini Ufaransa kwa kupokea dola milioni 2 kwa ajili ya kuufanya mji wa Rio kuwa muandaaji wa michuano ya Olimpiki mwaka uliopita.

Image caption Lamine Diack ameongoza shirikisho la riadha tokea mwaka 1999 mpaka 2015

Lamin kwa sasa anashikiliwa nchini Ufaransa na tiyari amenyanganywa hati yake ya kusafiria huku Papa Massata akiwa amejificha nchini kwao Senegal.

Awali wawili hao walikana mashitaka ya kuhusika katika rushwa hiyo.