Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 20.10.2017

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 29, amewaambia wachezaji wenzake kwamba atahamia Manchester United. (Mirror)

Real Madrid wako tayari kumtoa Karim Benzema, 29, kama sehemu ya ofa yao kutaka kumchukua mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24. (Daily Express - kupitia El Gol Digital)

Manchester United wanatarajiwa kuongeza mkataba wa kiungo wa kati Ander Herrera, 28, na pia wanasalia na matumaini ya kumshawishi kiungo wa kati Marouane Fellaini, 29, kusalia nao. (Express)

Meneja wa Burnley Sean Dyche hajasema kwamba hamezei mate nafasi ya umeneja Leicester. (Mirror)

Juhudi za Chelsea kumtafuta kiungo wa kati wa Roma Radja Nainggolan zimepigwa jeki baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuzungumza vyema kuhusu klabu hiyo ya Uingereza. (Star)

Real Madrid wanajutia kutomuuza fowadi Gareth Bale, 28, kwa Manchester United majira ya joto yaliyopita. (Diario Gol via Star)

Inter Milan wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Ramires, 30, mwezi Januari baada ya kuafikiana mkataba wa mkopo na klabu ya Ligi Kuu ya China Jiangsu Suning.(Gazetta dello Sport kupitia Mail)

Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Gareth Bale

Winga wa Bayern Munich Arjen Robben, 33, hana haraka katika mazungumzo kuhusu mkataba mpya licha ya kwamba mkataba wake wa sasa unafikia kikomo mwaka ujao. (Sky kupitia FourFourTwo)

Meneja wa zamani wa Chelsea Luiz Felipe Scolari anatarajiwa kuondoka Guangzhou Evergrande baada ya kuwa katika klabu hiyo ya China kwa miaka mitatu. (Mail)

Liverpool watakataa ofa zozote za kutaka kumnunua James Milner mwezi Januari. Mchezaji huyo wa miaka 31 amesalia kwenye mipango ya meneja Jurgen Klopp. (Telegraph)

Manchester United na Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Ujerumani Marco Reus, 28, lakini Borussia Dortmund wanataka kuendelea kuwa naye. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marco Reus

Beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte, 23, amesema alikataa juhudi za Manchester City na Chelsea kutaka kumnunua majira ya joto kwa sababu bado ameridhika kuwa katika klabu hiyo ya Uhispania. (L'Equipe kupitia Talksport)

Manchester United wanamnyatia kinda wa miaka 17 wa Benfica Umaro Embalo, 17. (Press Association - kupitia Sun)

Meneja wa Everton Ronald Koeman amesema kiungo wa kati Davy Klaassen, 24, anatatizika kutoa mchango kwenye klabu hiyo tangu ahamie huko kwa £25m majira ya joto. (Liverpool Echo)

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amepitwa na mwandishi wa hadithi za Harry Potter JK Rowling kama mtu mashuhuri katika michezo na sanaa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Forbes - via Goal)

Wachezaji wa Chelsea hawajafurahishwa na ukali wa mazoezi wanayofanyishwa na Antonio Conte na wana wasiwasi kwamba mazoezi hayo yanatatiza juhudi zao za kutetea taji na kuzidisha majeraha. (Times)

Mfanyabiashara Mwingereza Amanda Staveley amekuwa mtu wa tano kujitokeza kutaka kununua klabu ya Newcastle United, hata hivyo uuzaji wa klabu hiyo hautarajiwi kufanywa hivi karibuni. (Guardian)

Kiungo wa kati wa Watford Richarlison amefungua roho kuhusu ujana wake Brazil na amesema wakati mmoja aliwahi kukabiliwa na majambazi waliokuwa na bunduki. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Manchester United Nemanja Matic amesema Jose Mourinho ndiye mkufunzi mzuri zaidi ambaye amewahi kufanya kazi naye, amesema yeye ni kama "nembo" kivyake. (Elevate kupitia Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nemanja Matic

Wachezaji wa Leicester City wameghadhabika na wanataka majibu kuhusiana na uamuzi wa bodi ya klabu hiyo wa kumfuta kazi Craig Shakespeare, amesema kaimu meneja Michael Appleton. (Guardian)

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alionekana kumeza tembe ya kuongeza sukari mwilini wakati wa mechi waliyowashinda Olympiakos Jumatano. (Mail)

Mshambuliaji wa Southampton Nathan Redmond atatoa mchango kwa hisani kwa kila bao analofunga ao kusaidia kufunga msimu huu. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere kwa mara nyingine amemshutumu mshambuliaji wa Watford Troy Deeney baada ya ushindi wa Gunners katika Europa League.

Winga wa Liverpool Mohamed Salah naye alikataa jumba la kifahari alilokuwa anataka kupewa kama zawadi kwa kuwasaidia Misri kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao(Liverpool Echo)

Mada zinazohusiana