Roma washtakiwa kwa matusi ya 'tumbili' dhidi ya Antonio Rudiger

Antonio Rudiger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mamake Rudiger anatokea Sierra Leone

Roma wameshtakwia na Uefa baada ya baadhi ya mashabiki wake kusikika wakimuita beki wa Chelsea Antonio Rudiger tumbili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliingia kama nguvu mpya dakika ya 77 mechi ya Kundi C Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano uwanjani Stamford Bridge.

Rudiger, 24, alihamia Chelsea kutoka Roma majira ya joto.

Kesi hiyo itashughulikiwa na kamati ya maadili na nidhamu katika Uefa tarehe 16 Novemba.

Kabla ya kuhamia England kwa £29m, Rudiger alikuwa amesema ubaguzi wa rangi katika mechi Italia ni tatizo sugu.

Mada zinazohusiana