Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 21.10.2017

Barcelona inajiandaa kwa uhamisho wa mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 28. (Don Balon, via Daily Express)
Image caption Barcelona inajiandaa kwa uhamisho wa mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 28. (Don Balon, via Daily Express)

Barcelona inajiandaa kwa uhamisho wa mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 28. (Don Balon, via Daily Express)

United itanunua kandarasi ya mwaka mmoja ya Herrera iwapo atakataa kuweka kandarasi mpya na Manchester United mwishoni mwa mwaka huu. (Manchester Evening News)

Image caption Barcelona itajaribu mara ya mwisho kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Philippe Coutinho katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Daily Mirror)

Barcelona itajaribu mara ya mwisho kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Philippe Coutinho katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Daily Mirror)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa klabu hiyo inafanya bidii ili kumfanya kiungo wake wa kati Coutinho ajihisi kusalia katika klabu hiyo msimu huu. (Telegraph)

Image caption Mesut Ozil,

Kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, anataka kujiunga na Manchester United wakati kandarasi yake na Arsenal itakapokamilika mwishoni mwa msimu huu . (Daily Mail)

Ozil hajafanya mazungumnzo kuhusu kandarasi mpya na Arsenal tangu mwezi Machi lakini hajamwambia mtu yeyote katika klabu hiyo kwamba angependa kuhamia Old Trafford.(Sun)

Hatahivyo mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ana imani kwamba Ozil atasalia katika klabu hiyo asilimia "100% (Sky Sports)

Image caption Mashabiki wa Leicester

Uongozi wa Leicester City' utakutana na aliyekuwa mkufunzi wa Southampton Claude Puel huku wakimtafuta mrithi wa kocha waliyemfuta kazi Craig Shakespeare. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 24, anasema kuwa anataka kuichezea klabu moja pekee licha ya kulengwa na Real Madrid. (Daily Mirror)

Mkufunzi wa Spurs Mauricio Pochettino anataka kumsajili kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley 23-year-mnamo mwezi Januari kwa sababu klabu hiyo inakabiliwa na majeraha mengi. (Daily Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barcelona huenda ikataka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Andre Silva, 21, ambaye anaswaka na Arsenal (Sun)

Barcelona huenda ikataka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Andre Silva, 21, ambaye anaswaka na Arsenal (Sun)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anatarajia mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 36, atarudi kutoka kwa jeraha kabla ya kukamilika kwa mwaka huu . (Telegraph)

Arsenal, Chelsea na Manchester City wanapanga kumsajili kinda wa Ufaransa Lenny Pintor ,17, ambaye anaichezea klabu ya Brest. (Sun)

Mada zinazohusiana