Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.10.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Real Madrid wana matumaini ya kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, msimu ujao. (Sun on Sunday)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anammezea mate mchezaji wa Benfica Alex Grimaldo, 22. (Metro)

Manchester United wanajiandaa kumpa mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid na Brazil Casemiro, 25, mshahara mnono kumshawishi kuondoka Bernabeu ili aelekee Old Trafford. (Sunday Express)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anaweza kupata pauni miioni 500 kwa msimu ujao ikiwa mwanamke mfanyabiashara raia wa Uingereza Amanda Staveley atafanikiwa kukinunua klabu hiyo. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rafael Benitez

West Ham wanamtaka meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancin, kuchukua mahala pa Slaven Bilic ikiwa atashindwa kuboresha matokeo mabaya ya klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Barcelona wanajiandaa kumpa mkataba wa maisha mshambuliaji Lionel Messi,30, katika klabu hiyo. (ESPN FC)

Manchester United wanajaribu kumasaini mchezaji wa kiungo cha kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21 Carlos Soler, kutoka Valencia kwa kima cha dola milioni 30. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha EPA/REUTERS
Image caption Lionel Messi

Newcastle wanataka kumrejesha mchezaji wa kiungo cha kati ya wa Ufaransa Hatem Ben Arfa,30, kutoka Paris St-Germain. (Sun on Sunday)

Mshambuliaji Basel Dimitri Berlin, 20, amethibitisha kuwa alikataa ombi la kuhamia Manchester United mwaka 2014. (Metro)

Mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 21, anasema ana ndoto ya kuichezea Manchester United. (Sunday Mirror)

Mada zinazohusiana