Arsenal yainyoa bila maji Everton 5-2

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil alifunga bao la kwanza la Arsenal

Everton ilishuka katika ligi kuu baada ya kutandikwa mabao 5-2 na Arsenal katika uga wa Goodison Park.

Nacho Monreal, Mesut Ozil, Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey waliifungua Arsenal huku naye Wayne Rooney aliwafungia Everton bao lao la kwanza.

Oumar Niasse alifungua Everton bao la pili kabla ya Alexis Sanchez kuiongezea Arsenal bao la tano.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rooney aliifungia Everton bao la kwanza

Idrissa Gueye alitimuliia uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi ya njano mara mbili wakati Everton walikuwa chini kwa mabao 2-1.

Ushindi huo wa Arsenal ugenini uliipandisha ngazi juu ya Watford hadi nafasi ya tano katika jedwali huku Everton wakiwa hawajashinda katika mechi tano.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sanchez aliongeza Arsenal bao la tano