Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 23.10.2017

Mauricio Pochettino Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauricio Pochettino

Real Madrid wanamwinda Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino kuweza kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane. (Sun)

Arsenal wanatarajiwa kuanza mazungumzo na waakilishi wa Jack Wilshere kuhusu kuongezwa mkataba wa mchezaji huyo wa safu ya kati wa England kupita msimu ujao. (Daily Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibatahimovic,36, ana karibu miaka 5 au 6 hivi ya kucheza kandanda kwa mujibu wa ajenti wake Mino Raiola. (FourFourTwo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Henry Onyekuru

Everton wanatarajiwa kuongeza pesa zao maradufu kwa mlinzi Henry Onyekuru 20, ambaye alijiunga na Anderlecht kwa mkopo baada ya kuwasili uwanja wa Goodison Park, huku nao Juventus na Atletico Madrid wakimmezea mate Mnigeria huyo. (Sun)

Liverpool wana mpango wa kutoa pauni milioni 4.5 kwa mchezaji wa safu ya kati Manor Solomon wa miaka 18 ambaye ameonyesha mchezo mzuri akiichezea Maccabi Petah Tikva. (Sun)

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United na England Gary Neville, anasema kuwa hawezi kamwe kurejea kwenye usimamizi wa kandanda (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anasema ni vigumu kuamini kuwa Mesut Ozil anataka kuondoka klabu hiyo baada ya mcheza safu huyo wa kati raia wa Ujerumani, kuonyesha mchezo mzuri wakati Arsenal iliishinda Everton Mabao 5-2. (Metro)

Mshambuliaji wa Newcastle raia wa Uhispania Mikel Merino,21. yuko sawa kabisa kuweza kuwavutia Real Madrid na Barcelona (Independent)

Meneja wa Real madrid Zinedine Zidane amemuambia rais wa klabu hiyo Florentino Perez kuwa hataki mchezaji yeyote kuuzwa wakati wa msimu wa mwezi Januari. (Don Balon - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zinedine Zidane

Meneja wa Huddersfield David Wagner amefichua kuwa alisherehekea ushindi wa klabu yake dhidi ya Manchester United kwa mvinyo. (Daily Mirror)

Manchester United hawako wazuri kama Manchester City au Tottenham, kulingana na wing'a wa Huddersfield Tom Ince, 25. (Daily Star)

Mada zinazohusiana