Celtic waadhibiwa kwa sababu ya Mbappe

Shabiki alikimbia kuelekea kwa Kylian Mbappe uwanjani Celtic Park Haki miliki ya picha SNS Group
Image caption Shabiki alikimbia kuelekea kwa Kylian Mbappe uwanjani Celtic Park

Uefa wamewatoza Celtic faini ya £8,900 (euro 10,000) baada ya shabiki wao kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mchezaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu hizo mbili mwezi uliopita.

John Hatton amekiri mashtaka ya kutaka kumshambulia mtu mahakama ya liwali Glasgow.

Ni mara ya 12 katika miaka sita kwa Uefa kuiadhibu Celtic kutokana an vitendo vya mashabiki wake.

Julai, walitozwa faini ya £20,600 kutokana na bango lililowekwa wakati wa mechi yao dhidi ya Linfield.

Hatton, 21, kutoka Belfast aliruka uzio wa chuma na kumrushia teke Mbappe baada ya Edinson Cavani kufunga bao la tatu mechi ambayo Wafaransa hao walishinda 5-0.

Amepigwa marufuku kuhudhuria mechi zozote Uingereza na liwali Sukwinder Gill.

Paris St-Germain pia wametozwa na Uefa £4,450 (euro 5,000) kwa sababu ya viti vilivyoharibiwa wakati wa mechi hiyo 12 Septemba.

Mada zinazohusiana