Bravo awaokoa Man City mikononi mwa Wolves

Manchester City v Wolves Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City hawajashindwa mechi 14 msimu huu

Claudio Bravo aliwafaa sana Manchester City baada ya kuwasaidia kulaza Wolves kupitia mikwaju ya penalti katika Kombe la Carabao na kuwasaidia kufika robofainali.

Bravo, alifanya kazi ya ziada kuzuia wasifungwe bao muda wa kawaida wa mechi, na aliendeleza hilo kwa kuzuia mikwaju ya Alfred N'Diaye na Conor Coady wakati wa matuta ya baada ya mechi baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.

City walifunga mikwaju yao yote, mkwaju wa Sergio Aguero ukiwa wa ushindi.

Wolves walikuwa ndiyo timu ya kwanza kuwalemea viongozi hao wa Ligi ya Premia na kuwazuia kufunga msimu huu.

Wolves, wamo alama mbili mbele kileleni katika Ligi ya Championship na walicheza vizuri sana mechi hiyo iliyochezewa Etihad, wakishangiliwa na mashabiki wao wapatao 6,000.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wolves ndio wa kwanza Manchester City msimu huu kuwazuia City kufunga katika dakika 90 za mechi

Kabla ya kufika Etihad, vijana hao wa Nuno Espirito Santo walikuwa wamefungwa mabao 13 pekee katika michezo 16 msimu wote.

City watakuwa ugeninit West Bromwich Albion Jumamosi wakilenga kuendeleza ubabe wao Ligi ya Premia.

Wolves nao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya QPR uwanjani Loftus Road katika ligi ya Championship siku hiyo.

Mada zinazohusiana