Bristol City kukutana na Manchester United katika kombe la Carabao

Manchester United midfielder Jesse Lingard (left) Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Mchezaji wa Manchester United Jesse Lingard (kushoto) alifunga na kuisaidia timu yake kuishinda Swansea 2-0

Mechi za robo fainali ziliwakutanisha pamoja Bristol City na Manchester United, baada ya matatizo ya kiufundi kusababisha mashabiki kusubiri kwa hadi masaa mawili, baada ya matangazo hayo kushindikana kutangazwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Twitter.

Arsenal watakutana na West Ham, huku Leicester City wakiwa nyumbani na Manchester City nao Chelsea wakiwaalika Bournemouth.

Droo hiyo ilistahili kuonyeshwa moja kwa moja mwendo wa saa 16:00 BST.

Hata hivyo baada ya kushindikana mara kadhaa baadaye video yake ilitangazwa.

Ligi ya EFL na Twitter wote waliomba msamaha kwa kuchelewa kutangaza kwa takriban saa moja na sekunde 45.

EFL sasa imeomba kulezwa kwa kina kile kilisababisha warsha hiyo kuchelewa kutangazwa.

"Tunaomba msamaha kwa matatizo yaliyosababisha kuchelewa kwa droo ya raundi ya tano."

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea