Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 30.10.2017

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Paris St-Germain wamemuorodhesha mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, kuwa nambari moja kati ya wachezaji ambao wanalenga kuwasaini msimu ujao. (TF1 - in French)

Manchester City wanaamini kuwa wanaweza kumpata mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid, Isco, 25, licha ya yeye kusaini mkataba wa muda mrefu huko Bernabeu. (Don Balon, via Daily Express)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene wenger

Arsenal watampa mashambuliaji Eddie Nketiah, 18, mkataba mpya wa miaka mitano ambapo mshahara wake utakuwa kati ya pauni 2,000 hadi 15,000 kwa wiki. (Sun)

Huku Meneja wa Burnley Sean Dyche akihusishwa na kuchukua kazi huko Everton, mlinzi Stephen Ward amesema kumpoteza itakuwa pigo kubwa. (Times - subscription required)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption David Moyes

Ikiwa Dyche ataondoka, Burnley watajaribu kujaza nafasi yake na aliyekuwa meneja wa Everton na Manchester United David Moyes. (Sun)

Huenda meneja wa Sunderland Simon Grayson akafutwa ikiwa klabu yake haitaishinda Bolton siku ya Jumanne. (Daily Star)

Meneja wa Manchester United anasema kuwa hana uhakika ikiwa Paul Pogba atakuwa sawa kucheza. (Daily Mirror)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alexi Sanchez

Meneja wa Arsenal anasema kwa mshambuliaji Alexi Sanchez ana mkataba kuifanyia mema Arsenal wakati watacheza na Manchester City siku ya Jumapili. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale huenda akakosa mechi dhidi ya klabu yake ya zamani Tottenham katika Champions League siku ya Jumatano. (Times - subscription required)

Mada zinazohusiana