Katie Taylor kupanda ulingoni Desemba 15

Katie Taylor anasema huu ni mwanzo wa yeye kushinda mataji mengi ya kimataifa
Maelezo ya picha,

Katie Taylor anasema huu ni mwanzo wa yeye kushinda mataji mengi ya kimataifa

Bingwa mpya wa dunia wa mkanda wa WBA Katie Taylor anatarajiwa kutetea taji hilo la uzito wa kati Desemba 15 nchini Uingereza.

Taylor mwenye miaka 31 hakutarajiwa kupigana tena mpaka mwakani baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Anahi Sanchez siku ya Jumamosi ambapo alipata jeraha dogo.

Jeraha hilo linakaribia kupona na Taylor atarejea uwanjani licha ya kwamba sehemu na ni nani atayepigana nae bado havijawekwa wazi.

''Itakuwa kumaliza mwaka vizuri, ninaamini hivyo,''alisema Taylor.

Taylor ashinda pambano lake la kwanza la kimataifa dhidi Sanchez siku ya Jumamosi.