Van Niekerk kuikosa michuano ya Jumuiya ya madola 2018

van Niekerk alitarajiwa kutoa upinzani mkali katika michuano hiyo
Maelezo ya picha,

van Niekerk alitarajiwa kutoa upinzani mkali katika michuano hiyo

Mkimbiaji wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk ataikosa michuano ya jumuiya ya Madola ya 2018 baada ya kuumia goti wakati akishangilia.

Van Niekerk bingwa wa michuano ya mita 400 ya dunia na michuano ya Olimpiki alikua na nia ya kushiriki michuano ya mita 100 na 200 nchini Australia.

Kwa sasa atahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuweza kuwa fiti kuendelea na michuano mingine.

Michuano ijayo ya Jumuiya ya Madola itafanyika April 4 mpaka 15 katika mji wa Gold Coast nchini Australia.