Beki wa PSG aifungia timu yake Hat-trick

Beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa alikuwa mlinzi wa kwanza kufunga hat-trick huku timu yake ikiicharaza Anderlecht bao 5-0

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa alikuwa mlinzi wa kwanza kufunga hat-trick huku timu yake ikiicharaza Anderlecht bao 5-0

Beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa alikuwa mlinzi wa kwanza kufunga hat-trick huku timu yake ikiicharaza Anderlecht bao 5-0 na kuweza kufuzu katika mechi za muondoano za klabu bingwa Ulaya.

Kurzawa alikuwa amefunga mabao 17 pekee kabla ya mechi hiyo kuanza lakini akafunga mabao matatu katika kipindi cha pili.

Neymar na Marco Verratti pia walifunga bao kila mmoja wao huku PSG ikifuzu kwa urahisi katika timu 16.

Bayern Munich pia walifuzu baada ya kuilaza Celtic 2-1 katika mechi nyengine.

Kurzawa alionyesha ishara za mshambuliaji katika mabao yake mawili ya kwanza akifunga baada ya mpira kugonga mwamba na kurudi uwanjani na baadaye kufunga bao la pili kwa kichwa kabla kufunga bao lake la tatu katikati ya wachezaji wengi.