Tottenham yaichapa Real Madrid 3-1 yatinga 16 bora

Dele Alli alikuwa katika kiwango kizuri cha mchezo
Maelezo ya picha,

Dele Alli alikuwa katika kiwango kizuri cha mchezo

Dele Alli alifunga mara mbili na kushuhudia Tottenham Hotspur ikiichapa miamba ya Hispania na mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Ulaya Real Madrid na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora.

Real Madrid wamefungwa kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi tokea mwaka 2012.

Christian Eriksen aliiandikia Spurs goli la tatu na la ushindi na kuizamisha kabisa Madrid ambayo itahitaji kushinda michezo iliyosalia ili kufuzu hatua inayofuata.

Goli la Madrid lilipachikwa na Cristiano Ronaldo ambaye licha ya kufunga goli hilo hakuwa katika kiwango kizuri sana.

Spurs wamefikisha alama 10 huku Madrid ikiwa na alama 7.