Nadal kumaliza 2017 akiwa namba moja kwa ubora

Rafael Nadal alishinda vikombe vya French Open na US Open mwaka 2017
Image caption Rafael Nadal alishinda vikombe vya French Open na US Open mwaka 2017

Rafael Nadal atamaliza mwaka 2017 kwa rekodi ya kuwa mchezaji namba moja kwenye mchezo wa tenis baada ya kumshinda Hyeon Chung kwenye mzunguko wa pili katika michuano ya Paris Masters.

Nadal raia wa Hispania ambaye mwanzo wa mwaka huu alikuwa namba tisa katika viwango vya ubora na kuanza kupanda kupitia ushindi wa French na US Open ameshinda kwa seti 7-5 6-3 ikiwa ni ndani ya saa moja na dakika 48.

''Ilikuwa ngumu sana kwangu kutokea nyuma, katika majereha, sikucheza muda mrefu na sasa nipo hapa,'' alisema.

Nadal mwenye miaka 31 atacheza dhidi ya Pablo Cuevas wa Uruguay katika hatua ya 16 bora.