Wing Jonny kuukosa mchezo dhidi ya Argentina kutokana na majeraha

Wing Jonny May amekuwa katika kiwango kizuri na kuwa tegemeo kwa timu yake
Maelezo ya picha,

Wing Jonny May amekuwa katika kiwango kizuri na kuwa tegemeo kwa timu yake

Mchezaji muhimu Wing Jonny May wa Uingereza anaweza kuukosa mchezo dhidi ya Argentina kutokana na kuumia nyama za paja.

Mchezaji huyo anayetokea jiji la Leicester mwenye magoli 10 katika michezo tisa ameumia katika mazoezi ya timu yake huko Ureno.

May mwenye miaka 27 anaungana na Jack Nowell na Elliot Daly ambao wote ni majeruhi.

Mchezaji mwingine Marcus Smith nae pia anarejea nyumbani baada ya kuumia mguu.

Kutokana na majeraha yaliyokumba timu hiyo, mazoezi yamesitishwa ili kupata muda wa wachezaji kuwa sawa zaidi.