Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 02.11.2017

Antonio Conte

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antonio Conte

Meneja wa Chelsea Antonio Conte bado anaungwa mkono na bodi licha ya kipigo walichopata kutoka Roma siku ya Jumanne. (Mirror)

Everton wako tayari kulipa pauni milioni 2.5 za kuachiliwa meneja wa Burnley Sean Dyche. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ronald Koeman

Nuno Espirito Santo anatathmini ikiwa atachukua nafasi iliyo Everton kufuata kufutwa kwa Ronald Koeman, lakini pia anatarajiwa kusalia Wolverhampton Wanderers. (Guardian)

Aliyekuwa meneja wa Rangers Ally McCoist, anapania kuongoza Sunderland kufuatia kufutwa kwa meneja Simona Grayson. (Daily Star)

Mshambuliaji wa Gremio, Luan, 24, ambaye alikuwa akitafutwa na Barcelona, Liverpool na Arsenal amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Brazil hadi mwaka 2010. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho

Mameneja Mauricio Pochettino wa Tottenham, Antonio Conte wa Chelsea na Jose Mourinho wa Manchester United huenda wakawa kwenye orodha ya wale wanaosakwa na Paris St-Germain. (Paris United - in French)

Barcelona wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji Timo Wener, 21, na mlinzi Dayot Upamecano, 19, kutoka RB Leipzig. (Mundo Deportivo via

Meneja wa Southend, Phil Brown anasema kuchukua usukani huko Sunderland inaweza kutumiza ndoto yake (Basildon, Canvey and Southend Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amekana uvumi wa kuihusisha Arsenal na kuhama kwa wing'a wa Monaco Thomas Lemar. (Evening Standard)

Wenger anataka kukamilisha mazungumzo ya mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati, Jack Wilshere, ifikapo Disemba. (Mirror)