Aguero avunja rekodi huku ManCity wakiicharaza Napoli 4-2

Sergio Aguero amekuwa mfungaji wa mabao mengi katika historia ya klabu ya Manchester City huku timu hiyo ikiilaza Napoli 4-2 ugenini

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Sergio Aguero amekuwa mfungaji wa mabao mengi katika historia ya klabu ya Manchester City huku timu hiyo ikiilaza Napoli 4-2 ugenini

Sergio Aguero amekuwa mfungaji wa mabao mengi katika historia ya klabu ya Manchester City huku timu hiyo ikiilaza Napoli 4-2 ugenini na kutinga raundi ya muondoano katika mechi ambayo ilikuwa na mbwembwe za kila aina.

City ilitoka nyuma na kuweza kushinda katika mechi kati ya timu zinazofunga sana na ambazo zilikuwa hazijafungwa katika ligi ya Uingereza na ile ya Serie A.

Napoli waliongoza katika dakika za kwanza 30 na walifaa kuongoza baada ya Lorenzo Insigne kucheza nipe ni kupe na Dries Maertens na kumfunga kipa Ederson.

City walianza kutawala mchezo baada ya mchezo mzuri na walisawazisha wakati Otamendi alipofunga krosi iliopigwa na Iikay Gundogan ambaye aliwashangaza wengi alipoanzishwa.

Hatahivyo ni ufungaji mabao wa Aguero dhidi ya Napoli siku ya Jumatano ambao ulimfanya kuipita rekodi ya mabao iliowekwa na Eric Brook ya mabao 177 katika mashaindano yote aliyochezea City na anaongoza kwa wingi wa magoli katika klabu yake akiwa na mabao 178.