Arsenal yabanwa mbavu na zvezda

Wachezaji wakimenyana katika mchezo huo
Maelezo ya picha,

Wachezaji wakimenyana katika mchezo huo

Arsenal imekubali kubanwa mbavu na klabu ya FK Crvena zvezda ya Serbia kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.

Licha ya Arsenal kulisakama lango la zvezda kwa muda mrefu lakini hawakufanikiwa kupata goli huku mara kadhaa Olivier Giroud na Jack Wilshere wakishindwa kufunga pia.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amewatumia wachezaji wengi ambao sio wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya kujilinda na mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya vinara wa ligi hiyo Manchester City.

Maelezo ya picha,

Giroud alifunga goli la ushindi katika mchezo wa awali

Baada ya mchezo huo Wenger amesema zvezda sio ya kubeza na hakuna timu inayokubali kupoteza kirahisi.

Arsenal inaongoza katika kundi H kwa kuwa na alama 10 ikifuatiwa na zvezda yenye alama 5.