Victoria Azarenka kuikosa michuano ya kombe la Fed

Azarenka alikosa pia michuano ya US Open mwezi Agosti
Image caption Azarenka alikosa pia michuano ya US Open mwezi Agosti

Victoria Azarenka wa Belarus ataikosa michuano ya kombe la Fed dhidi ya Marekani kwa sababu bado anashughulikia suala la mtoto wake mdogo aliyezuiliwa Marekani.

Azarenka alijitoa kwenye michuano ya US Open mwezi Agosti baada ya kushindwa kumuacha mtoto wake Leo mwenye miezi 10 jijini California baada ya Jaji kuamua anapaswa kusalia hapo wakati mustakabali wake ukijadiliwa.

''Inaumiza lakini hatuwezi kubadilisha jambo lolote kwa sasa,'' alisema nahodha wa Belarus Eduard Dubrov.

Michuano hiyo inaanza Movemba 11 mjini Minsk.

Azarenka hajacheza tokea alipofungwa na Simona Halep mwezi Julai.

Kwa sasa matumaini makubwa ya Belarus yapo kwa Aryna Sabalenka.