Everton yabanduliwa kombe la Yuropa

Everton iliosalia na wachezaji 10 uwanjani walidondolewa katika kombe la ligi ya Yuropa baada ya kushindwa na Lyon

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Everton iliosalia na wachezaji 10 uwanjani walidondolewa katika kombe la ligi ya Yuropa baada ya kushindwa na Lyon

Everton iliosalia na wachezaji 10 uwanjani walibanduliwa katika kombe la ligi ya Yuropa baada ya kushindwa na Lyon huku matumaini ya kocha David Unsworth ya kupewa kandarasi ya kudumu kama meneja yakipata pigo kubwa.

Kushindwa huko mbali na sare ya 1-1 kati ya klabu ya Atalanta na Apollon Limassol kunamaanisha kwamba The Toffees hawaezi kusonga mbele huku ikiwa imesalia mechi mbili.

Unsworth, ambaye alipandishwa daraja kutoka taasisi ya soka ya klabu hiyo kama kaimu mkufunzi baada ya kufutwa kwa Ronald Koeman sasa amepoteza mechi zote tatu allizosimamia.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Bertrand Traore alianza kufunga kunako dakika ya 68 baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Everton na kumfunga kipa Jordan Pickford.

Bao lao la pili lilijiri dakika 14 baadaye kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo baada ya mchezaji wa ziada Houssem Aouar kumwacha bila jibu kipa huyo wa Uingereza.

Lakini mambo yaliendelea kuwa mabaya zaidi kwa wageni hao wakati waliposalia wachezaji kumi baada ya Morgan Schneiderlin kupata kadi ya njano ya pili kwa kumchezea visivyo Maxwel Cornet.

Na huku ikiwa imesalia dakika mbili mchezaji wa Man United Memphis Depay alifunga bao la tatu na la mwisho kupitia kichwa akiwa maguu sita karibu na goli.