Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 03.11.2017

Mkufunzi wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane
Image caption Mkufunzi wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane

Real Madrid Italenga kumuajiri mkufunzi wa Tottenham manager Mauricio Pochettino kama chaguo lao la kwanza kuchukua mahali pake Zinedine Zidane. (Daily Mail)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abrahamovic tayari ameamua kumfuta kazi meneja Antonio Conte. (Marca)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumwachilia Luke Shaw mwenye umri wa miaka 22 kundoka katika klabu hiyo mwezi Januari ,wakati ambapo wawili hao hawazungumziani. (Sun)

Image caption Mkufunzi wa klabu ya Man United Jose Mourinho

Shaw yuko tayari kurudi kwa klabu yake ya zamani Southampton, huku klabu hiyo ya Kusini mwa pwani ya Uingereza ikitarajiwa kumuuza beki Ryan Bertrand, 28, kwa klabu ya Manchester City. (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Watford Stefano Okaka, 28, hajaelezea ni kwa nini aliwachwa nje na timu hiyo katika kipindi cha miezi miwili iliopita. (Watford Observer)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, anataka kucheza kwa muda mrefu katika klabu hiyo . (Sky Sports)

Hatma ya mshambuliaji wa City Sergio Aguero haijulikani huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akisema ''hajui ni lini kandarasi yake itakwisha''. (Goal)

Aguero anaamini kwamba kikosi kipya cha Manchester City's ni bora zaidi kuwahi kucheza nacho tangu kujiunga na klabu hiyo ya Etihad Stadium. (Times - subscription required)

Image caption Aguero anaamini kwamba kikosi kipya cha Manchester City'

Arsenal inakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Newcastle katika kumsajili kiungo wa kati wa Atalanta Miguel Almiron (Calciomercato, via Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, amesisitiza kuwa hajaishinikizi bodi ya klabu hiyo kumpatia kandarasi mpya ilioimirika. (Goal)

Wolfsburg inajaribu kuwailisha ombi la kutaka kumpatia usajili wa kudumu mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22-year Divock Origi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Liverpool. (ESPN)

Image caption Liverpool iko tayari kumpoteza kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can ,23,

Liverpool iko tayari kumpoteza kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can ,23, huku mazungumzo kuhusu kandarasi mpya yakikwama mwishoni mwa msimu huu. (Daily Mirror)

Winga wa Valencia's mwenye umri wa miaka 20 Goncalo Guedes hajui hatma yake ya iwapo atasalia katika klabu Paris St-Germain au la. (ESPN)

Arsenal inalenga kumsajili nyota wa Napoli Jorginho.

Machezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hatahivyo hajulikni iwapo anaweza kuondoka katika klabu hiyo ya Serie A mnamo mwezi Januari. (Transfer Market Web, via Daily Star)

Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Arsenal pia iko tayari kumnunua winga wa Chelsea ambaye hachezeshwi Charly Musonda, 21

Arsenal pia iko tayari kumnunua winga wa Chelsea ambaye hachezeshwi Charly Musonda, 21. (Foot Mercato, via Daily Mail)

Harry Redknapp amesema kuwa huenda akavutiwa na kuifunza klabu ya Sunderland ambayo haina kocha kufikia sasa. (Talksport)

Image caption Kiungo wa kati wa Schalke's 22 Leon Goretzka ameamua kukamilisha kandarasi yake na kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu huu

Kiungo wa kati wa Schalke's 22 Leon Goretzka ameamua kukamilisha kandarasi yake na kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu huu.(Mundo Deportivo - in Spanish)

Mtaalamu wa data katika klabu ya Fulham Craig Kline aliwaita maafisa wa polisi katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo baada ya kufutwa kazi. (London Evening Standard)

Mkurugenzi wa klabu ya RB Leipzig Ralf Rangnick anasema kuwa kiungo wa kati wa Liverpool Naby keita , 22, ni miongoni mwa wachezaji bora ambao amewahi kufanya kazi naye . (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa klabu ya Red Star Belgrade Richmond Boakye

Mshambuliaji wa klabu ya Red Star Belgrade Richmond Boakye ana hamu ya kujiunga na klabu ya Chelsea katika dirisha la uhamisho mwezi Januari. (London Evening Standard)

Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois anasema kuwa kiungo wa kati Nemanja Matic, 29, alikuwa na hamu ya kujiunga na Manchester United msimu uliopita hatua ambayo ingekuwa vigumu kwa Chelsea kumzuia. (Independent)

Mada zinazohusiana