Arsenal kumteua Montemuro kuwa meneja mpya

Joe Montemuro kuteuliwa na Arsenal
Maelezo ya picha,

Joe Montemuro kuteuliwa na Arsenal

Klabu ya Arsenal upande wa wanawake inatarajiwa kumteua mkufunzi Joe Montemuro kama meneja wake mpya kufuatia kuondoka kwa Pedro Martinez Losa.

Montemurro mwenye umri wa miaka 48 ni naibu mkufunzi wa klabu ya Ligi A Melbourne City.

Msimu uliopita alioongoza Melbourne City kushinda taji la ligi hiyo ya wanawake katika mwaka wa kwanza huku akimaliza msimu huo bila kufungwa.

Mkufunzi wa klabu hiyo ya Arsenal raia wa Uhispania Losa aliondoka katika klabu hiyo tarehe 25 mwezi Oktoba baada kuhudumu kwa miaka mitatu katika kikosi hicho.

Naibu kocha Ismael Garcia anafunza klabu hiyo kwa muda .