Manchester City kuchuana na Arsenal, wakufunzi wanasemaje?

Mshambuliaji wa Manchester City Aguerro akikabiliana na mwenzake wa Arsenal Sanchez
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Manchester City Aguerro akikabiliana na mwenzake wa Arsenal Sanchez

Manchester City hawana wachezaji waliopata majeraha mapya lakini Pep Guradiola huenda akataka kubadilisha kikosi chake kufuatia uhsindi wao wa Jumatano dhidi ya Napoli.

Mshambuliaji Gabriel Jesus alicheza dakika tano pakee kama mchezaji wa ziada nchini Italy na huenda akarudi pamoja na Kylie Walker na David Silva.

Beki wa kushoto wa Arsenal Sead Kolasinac anatarajiwa kukabiliana na jeraha la kiuno ili kuanzishwa baada ya kuguchia akiwa Swansea wikendi iliopita.

Shkrodan Mustafi, Santi Carzola , Danny Welbeck na Calum Chambers wanauguza majeraha.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake haitoweza kuvunja rekodi ya mechi 49 bila kufungwa inayoshikiliwa na Arsenal na akamtaka meneja wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi.

''Ningependa kumwania Wenger kwamba rekodi hiyo ni yake hatutaweza kuivunja. Asiwe na wasiwasi'', alisema Guradiola.

Naye meneja Arsene Wenger amesema kuwa kikosi chake kina fursa kuonyesha kwamba kinaweza kukabiliana na mechi kama hizo.