Chelsea kukabiliana na Man United, Conte asema ManCity ndio tatizo

Chelsea kukabiliana na Manchester United, Conte asema ManCity ndio tatizo
Maelezo ya picha,

Chelsea kukabiliana na Manchester United, Conte asema ManCity ndio tatizo

Chelsea inamkaribisha tena kiungo wa kati N'Golo Kante, ambaye amerudi katika mazoezi baada ya kuwa nje kwa mechi sita na jeraha la nyonga.

Victor Moses anaendelea kuuguza jereha lakini nahodha Gary Cahill ni sharti aanze baada ya kukosa kushiriki katika mechi ya ushindi dhidi ya Bournemouth.

Jesse Lingard hatoshiriki mechi hiyo baada ya kutelewa nje katika mechi dhidi ya Benfica kutokana na tatizo la mgongo.

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte: Sasa kuma matatizo makubwa kwa timu zote ambazo zinapigania kushinda taji la ligi ya Uingereza.Tatizo hilo ni Manchester City.Iwapo City itaendelea ilivyo itakuwa vigumu kwetu sisi kuwania taji hilo.lazima tujaribu kufanya vyema.

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho: Nataka kukiri kwamba kuna tofauti kubwa lakini mwishowe nataka kumaliza nikiwa mshindi kama vile nilivyoshinda nikiwa na Inter Milan.Wanataka kushinda kama walivyofanya msimu uliopita na ni siku moja tu.