Manchester City yaikung'uta Arsenal 3-1

Sergio Aguero scores a penalty
Maelezo ya picha,

Manchester City yaikung'uta Arsenal 3-1

Manchester City waliwakung'uta Arsenal 3-1 na kufungua mwanya wa pointi kileleni mwa ligi ya Premier.

Bao la Kevin de Bruyne na penalti ya Sergio Aguero iliiweka Man City katika nafasi ya kushinda ligi ya tisa.

Licha ya Alexandre Lacazette kuipa Arsenal bao la kuvuta machozi, Gabriel Jesus aliipa Manchester ushindi kwa kuifungia bao la tatu.

Arsenal huenda wangepata kipigo zaidi isingekuwa ni jitihada za kipa Petr Cech

Mafanikio ya Manchester City dhidi ya Machester United walio nafasi ya pili yatatokana na matokeo ya leo dhidi ya Chelsea.