Sock atwaa taji la Paris Master

Tenesi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Sock mshindi wa taji la Paris Masters.

Mchezaji namba 22 kwa ubora Jack Sock ametwaa taji lake la kwanza la Paris Rolex Masters kwa kumshinda Filip Krajinovic.

Sock alishinda mchezo huo wa fainali akitoka nyuma baada kufungwa seti ya kwanza kwa 7-5,kisha akashinda seti mbili za mwisho kwa 6-4 na 6-1dhidi ya Pilip.

Mchezaji huyo anakuwa Mmarekani wa kwanza kutwaa taji hilo toka alivyotwaa Andre Aggasi Mwaka 1999.

Sock ataingia katika nafasi kumi za juu za ubora wa viwango vya zinazotolewa leo jumatatu.